Historia yetu…
Tacmen Saccos ni Chama cha Ushirika cha Kuweka Akiba na Kukopa cha WANAUME WAKRISTO kutoka madhehebu mbali mbali bila ubaguzi wala uchaguzi.
Ili kuwa mwanachama, unatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:
- Uwe Mwanaume Mkristo mwenye mwendendo mzuri kwenye jamii na asiye na shutuma au mwenye jinai na uwe na umri usio pungua miaka 18,
- Uwe tayari kusoma, kuelewa na kufuata masharti ya ushirika wetu ambayo unaweza kupewa na uongozi – angalia link ya wasiliana nasi kwa blogu hii,
- Utakapo kuwa tayari kujiunga nasi, utamtumia afisa wetu kitambulisho chako na yeye atakutengenezea usajili kwenye chama na benki yetu kisha utalipia kama ifuatavyo:
- HISA 10, kila moja Tsh 20,000 sawa na Tsh 200,000/-
- AKIBA utaweka jumla ya Tsh 120,000/-
- KIINGILIO utaweka Tsh 25,000/- (kitalipwa mara moja tu)
- MICHANGO utaweka Tsh 60,000/- (sawa na Tsh 5,000/- kwa mwezi)
- HISA, AKIBA na MICHANGO unaweza kuruhusiwa kulipa nusu ya hizo zilizoandikwa hapo juu No.3, kisha ukamalizia zilizobaki ndani ya miezi mitatu.
- Utaruhusiwa kukopa baada ya kukamilisha uanachama na kuwa mwanachama kwa miezi mitatu.
KARIBU SANA UJIUNGE NASI!!!
