

Historia yetu…
Kati ya September 2014 na March 2015 tulikuwa na chakula cha jioni na mazungumzo kama wanaume wakristo peke yetu. Mazungumzo haya yalikuwa mazuri na yenye manufaa sana kwa wanaume wengi na waliyafurahia na kutamani yaendelee.
Ili kuendeleza haya mazungumzo na kuhusisha wanaume wengi zaidi, ndipo iliamuliwa kuwa whatsapp group ianzishwe. Tar 11 March 2015 whatsapp group ilianzishwa rasmi na Mwalimu Timoth Kyara na tukaanza kualika wanaume wakristo wengi.
Tulipokuwa kwenye mchakato wa kuanzisha group la whatsapp rasmi ndipo mapendekezo yaliletwa na jina TACMEN likapitishwa kuwa jina letu rasmi likiwa na maana ya Tanzania Christian Men Network!
Mazungumzo na mijadala iliendelea kwa kukutana mwisho wa wiki na pia kwenye mtandano kwa njia ya whatsapp mpaka mwaka 2016 tulikuwa na zaidi ya wanaume 200 kwenye group la whatsapp.
Hatimaye mazungumzo yalianza kuhusu kuwa na “Legacy” yetu, kumbukumbu, ya wanaume wakristo Tanzania. Baada ya mjadala muda mrefu ndipo ikakubalika kuwa tuwe na mahali petu, Real Estate Project, ambapo tutapaita ‘City of God – a Place of Peace and Harmany‘ hiyo ilikuwa August, 2016.
Hata hivyo, ili kufikia kwenye mradi wa City of God ni parefu na hivyo tukasema tunahitaji kuwa na Benki yetu ya wanaume wakristo.
Na kwa vile hatukuwa na fedha za kuanzisha benki, ikaonekana njia rahisi ya kuanza safari yetu ni kuanza na kitu ambacho tunaweza – Saccos.
Na hapo ndipo wazo la Saccos lilianza na mchakato wa kusajili na kuanzisha ukaanzishwa rasmi mwaka 2016.

Leave a comment