Mwanzo Mgumu
Baada ya kukubaliana kuanzisha rasmi Saccos mwaka 2016, tulianza rasmi mchakato wa kusajili na baada ya zaidi ya mwaka mmoja, Mnamo October 2017 tulipata usajili kama chama cha ushirika DSR-1644 Wilaya ya Kinondoni.
Ofisi yetu ya Mwanzo ilikuwa kwenye magari yetu na hasa gari la Mosses Samora Raymond Mduka na Timoth Japhethy Kyara na hatimaye tulipata ofisi pale karibu na Mwenge ambapo Ndugu Godfray Mkaikuta alikuwa mwanachama wa kwanza kujitolea kuwepo ofisini.
Usajili wetu usingekamilika kama isingekuwa juhudi na jitihada za nguvu sana za ndugu yetu Hamisi Akwilini Ndulu. Tunamshukuru sana yeye pamoja na viongozi wa ofisi ya Ushirika Kinondoni kutuwezesha kukamilisha ndoto hii na safari yetu kuanza na watu 25 na chini ya Tsh milioni Tano benki ya CRDB Ngome.



Leave a comment